Wafanyakazi wa kampuni ya BMBC wathibitisha kwamba umoja wao kazini uliwaletea maendeleo na kukiwa shida yoyote wanashirikiana kulitatua.
Katika mahojiano na kitengo cha kutoa habari cha BMBC walisema kwamba wanafanya kazi yao kwa bidhii, umoja na ushirikiano.
Wafanyakazi hao wanasema kwamba kufanya kazi kwa ushirikiano vinasababisha kazi kusonga mbele kwa muda uliopangiwa kazi hiyo.
Mumoja katika wafanyakazi hawo alisema:«Umoja ni nguvu ,penye umoja na ushirikiano kazi hufanywa vizuri.» Walisema kwamba kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano vinanufaisha kampuni kupata maendeleo na hivo nyumba inajengwa ipasavyo na kufurahisha mteja.