Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya BMBC anafahamisha kwamba mashirika ya kujiendelesha maaurufu cooperatives yanapaswa kuweka mbele kupewa elimu ili ajiendeleshe ipasavyo.
Mkurugenzi wa BMBC alisema hayo tarehe 8 Disemba 2021,katika mkutano wa wakuu wa mashirika hayo katika taarafa ya Ntahangwa mjini Bujumbura,walipokuwa wanapewa elimu.
Huwo mkurugenzi alisema tatizo la mashirika ya kujiendelesha ni kuwa yanatumia miradi ilioundwa na wengine badala ya kutumia miradi yao binafsi.
Mkurugenzi wa BMBC alisema: «Msitumie miradi ya wengine,andaa miradi yenu binafsi na muyitimize !»
Aliongeza kuwa ni vema mtu kuandaa mradi wake binafsi na kutoa maoni kwa wengine.
Mkurugenzi wa BMBC alisema ya kwamba mtu anapoandaa mradi ni ishara ya upendo kwa jamii na kwa nchi yake.
Mkurugenzi huwo wa BMBC alimaliza kwa kutoa wito kwa wakuu wa mashirika ya kujiendelesha kufahamisha kazi za mashirika yao kupitia mitandao ya kijamii.