Mmoja katika wafanyakazi wa kampuni ya BMBC anafahamisha kwamba tangu ajiunge na kampuni hiyo ameshanufaika mambo mengi sababu anapewa mshahara kulingana na kazi alioyoyifanya.
Katika mahojiano na gazeti la BNP Media, alisema kwamba alisomea usimamizi wa kazi za ujenzi ila alipofika BMBC alifundishwa kila kitu mpaka akafikia hatua ya leo ambapo anasimamia majengo yanayojengwa.
Mfanyakazi huwo alisema kwamba BMBC ilimuandaa katika kipindi cha miaka miwili ambapo alipewa mafunzo katika vitu mbali mbali vya ujenzi.
Alielezea gazeti hilo kuwa amefaidika vitu vingi tangu afike katika kampuni ya BMBC hasa kuhusu kujiendelesha kimaisha tofauti ya kabla na kujiunga na kampuni hiyo.
Katika siku zijazo,mfanyakazi huwo anatumaini kusimamia majengo mengi pamoja na pia ana mipango ya kuunda familia.