Mkuu wa kampuni ya BMBC anafahamisha kuwa mradi wa BMBCHOMES unakamilishwa katika kiwanja kizuri sana.
Katika mahojiano na kitengo cha kutoa habari alisema kwamba kuona benki ilikubali kuunga mkono mradi huwo ni ishara inayoonyesha uzuri wa mradi huwo.
Mkurugenzi huwo anasema kwamba katika mradi huwo wa BMBCHOMES,nyumba zipo bei nafuu ukilinganisha jinsi zitakazokuwa na vitu vitakavyokuwa ndani.
Mkurughenzi mkuu wa BMBC anasema hawana mpango wa kunufaika hela nyingi ila ni kwa ajili ya kufanya iwezekanavyo ili mradi huo mpya nchini ukamilike.
Vitu vitakavyokuwa ndani ya nafasi hiyo ni nyumba za kisasa zenye kujengwa vizuri,kutakuwa maji,barabara na umeme.
Vitu vingine ni uwepo wa internet,aina ya kuchunga usalama pamoja na aina ya kupewana habari bila kutoka nje ya chumba cha nyumba.
Kuhusu ununuaji wa nyumba,mtu akisha saini makubaliano ya ununuaji atalipa asilimia 20 ya bei ya nyumba kisha benki itaanza kutimiza malengo yake.
Mkurugenzi wa BMBC anamaliza na kusema kwamba baada ya miezi baada ya makubaliano na kulipa asilimia 20 ataingia nyumba na kuanza kuilipa baada ya mwezi kwa kipindi cha miaka 10.