Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya BMBC anafahamisha kwamba kazi nyingi ambazo kampuni ilipata zilisababisha kutopata muda wa kuweza kutoa habari za kampuni ili wateja waweze kufahamu yanayojili kwa kampuni hiyo.
Katika mahojiano na kitengo cha kutoa habari cha BMBC,mkurugenzi huwo alisema kwamba alikuwa hatowi habari zinazohusu kampuni hiyo sababu ya majukumu mengi ya kampuni aliokuwa anayasimamia.
Mkurugenzi huwo wa BMBC anasema kwamba kampuni anayoyiongoza ilipata miradi na kazi nyingi kutoka kwa wateja hivyo vikasababisha kukosa muda wa kutoa habari kwa wateja.



Alisema: “Tulipata majukumu mengi,kampuni imepanuka,kazi zimekuwa nyingi hivyo vyote vilituchukua muda wa kutosha.”
Mkurugenzxi mkuu wa kampuni ya BMBC anamaliza akisema kwamba hata kama hakutoa habari kwa wateja, walikuwa na fursa ya kuona habari mbali mbali za kampuni kupitia mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo.