Watu wengi kutoka sehemu mbali mbali wanaendelea kutembelea kampuni hiyo baada ya uzinduzi wa mradi wa BMBCHOMES2021.
Katika wanaotembelea shirika hilo, wamoja wanakuwa wametumwa na familia zao zenye kuishi nje ya nchi kabla ya kuamua kujiunga na mradi mpya wa BMBCHOMES2021.
Siyo tu wanaoishi nje ya nchi wanaotuma wakwao , na wenye kuwa nchi kati kati nao wanakuja kuuliza mradi huo,vinaonyesha ishara ya kuwa mradi huo ulipendwa na watu wengi na utawanufaisha siku zijazo.
Kitengo cha kutoa habari cha BMBC kinasema kwamba maongezi kati ya BMBC na wateja wa BMBCHOMES2021,yanaonyesha kuwa mradi huo umependwa sana na utakuwa wa kuridhisha kwa watu watakaoishi ndani ya mtaa huo.