Kampuni ya BMBC inasema kwamba watu wenye kuanzisha miradi yao wanapotumia miradi ya watu wengine mara nyingi wanapata hasara sababu wanakuwa hawajuwi jinsi miradi hiyo ilivyoandaliwa na wenye kuianzisha.
Katika mahojiano na kitengo cha kutoa habari cha BMBC,mkurugenzi wa BMBC alisema kwamba watu wengi siku hizi wanaandaa miradi iliofanywa na watu wengine kuliko kuanzisha miradi yao binafsi.
Mkurugenzi huwo anasema kwamba ingekuwa vizuri watu wakiachana na tabia ya kuiga miradi ya wengine sababu vinaweza kuwasababishia kupata hasara wasioyitegemea.

Mkurugenzi wa BMBC alisema: “Anaeandaa mradi asiige mradi wa mtu mwingine sababu hajuwi jinsi ulivyoandaliwa ndo sababu wengi wanapata hasara kwa njia hiyo.”
Mkurugenzi huwo anashauri watu kuachana na tabia ya kufanya miradi ya watu wengine.