Wafundi wa kampuni ya BMBC walionyesha kuwa kubomoa majengo ambayo yalijengwa bila kufuata taratibu na sheria za ujenzi, vilisababishwa na waliojenga kimakosa bila sababu yoyote.
Mkurugenzi wa kampuni ya BMBC alitufahamisha kwamba walichukuwa msemo wa BMBC baada ya kugundua kuwa kuna watu ambao wanajenga nyumba zitakazobomoa. Na msemo huwo ni «Munapojenga,jenga vizuri.» sababu kuna watu wanaojenga bila kufuata sheria na utaratibu za ujenzi.
Mkurugenzi huo anaongeza kwamba kuna waliojenga kimakosa bila sababu, ambapo walikuwa wanavamia sehemu zilizotengwa na serikali wakisahau kuwa nchi itapahitaji muda wowote.
Mkurugenzi wa BMBC anashauri watu wanaotaka kujenga kufuata sheria na taratibu za ujenzi. Hivo hata wakipigwa faini isiwe yakubomolea. Anaomba pia watu washirikishe wafundi wenye uzoefu ili wahudumiwe ipasavyo na waepuke kujenga kimakosa.