Mkuu anayehusika na wafanyakazi wa kampuni ya BMBC anasema kwamba wafanyakazi wa BMBC wanajitoa kufanya kazi na wanatimiza ipasavyo shughuli zao.
Katika mahojiano na kitengo cha kutoa habari cha BMBC,mkuu wa wafanyazi wa BMBC alisema kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wanajitoa ipasavyo sababu kuna wanaofika kazini kabla ya masaha na wengine wanaopitiliza masaa ya kazi mpaka jioni.
Mkuu huwo alisema kwamba alioanza kazi ya kuwa mkuu wa wafanyakazi wa BMBC ilikuwa kazi nugmu sababu kutoa sheria kwa mtu aliyekuwa mkuu wako siyo rahisi.
Alisema :« Kutoa sheria kwa mtu aliyekuwa anakusimamia siyo rahisi hata kidogo.»
Mkuu huwo anafahamisha kwamba alijiunga na BMBC akiwa fundi msaidizi baadaye akapanda cheo akawa fundi na hivi sasa ni mkuu wa wafanyakazi wote wa kampuni ya BMBC.
Mkuu wa wafanyakazi wa BMBC anatoa wito kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kufanya kazi vyema na bidii ili shirika ipate maendeleo.