Kazi na majukumu vya kampuni ya BMBC vinaonyesha kuwa kampuni hiyo ina wafundi na watalamu wenye ujuzi tofauti kwenye fani zinazohitajika katika ujenzi mpaka nyumba iweze kujaa ikiwa ya kawaida ao ghorofa.
Kampuni ya BMBC katika kazi zake za kila siku haihitaji watalamu kutoka nje ya kampuni sababu ina wafanyakazi wake wanaohitajika katika kila kitu kinachohusu ujenzi wa nyumba mpaka ikamilike.




Wafanyakazi wa kampuni hiyo wanaendelea kufanya jitihada kwa kuhudumia ipasavyo wateja wake wa kampuni kama kawaida.
Kampuni hiyo inatoa wito kwa watu wenye mipango ya ujenzi kushirikiana nayo ili iwatimiziye miradi yao ya ujenzi.